Header

Sahau kuhusu M-Pesa,Airtel Money na Tigo Pesa: Sasa unaweza kutuma na kupokea pesa kupitia Gmail

Sahau kabisa kuhusu M-Pesa,Airtel Money na Tigo Pesa kwani najua ukiwa na Gmail unauwezo wa kutuma ujumbe mfupi, picha na file mbalimbali kwa kutumia programu ya gmail lakini je unaonaje sasa ukiweza kutuma pesa kwa kutumia programu yako ya Gmail ya mfumo wa Android.?

Habari nzuri ni kwamba Google kupitia programu yake ya Gmail ya mfumo wa Android sasa inakuwezesha kutuma pesa kwa kutumia programu yako ya gmail. Google inakuwezesha kufanya yote hayo kwa kuunganisha na huduma ya Google Wallet ambapo ndio itakuwezesha kutuma pesa pale unapotaka kutuma barua pepe yako.Tamaza video ya kuona jinsi unavyoweza kutuma pesa kupitia akaunti yako ya Gmail

Kwa sasa huduma hii haipatikani kwa tanzania lakini inategemewa kuja kwenye siku za usoni hivyo endelea kutumia programu yako ya Gmail uku ukitembelea Tanzania Tech kila siku ili kupata habari za sehemu hiyo mpya pindi itakapo kuja kwa hapa Tanzania.

Comments

comments

You may also like ...