Header

Ukiachana na muziki wa Rap Jay Moe ataja wimbo wake bora wa injili wa muda wote

Msanii mkali wa bongo fleva Kutoka sinza Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ ambaye anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake ‘Nisaidie kushare’ huwezi amini ni mmoja kati ya msanii wa Bongo fleva mwenye mapenzi kati ya nyimbo kubwa za ijili kutoka Tanzania.

Akipiga stori na Twenzetu ya Times Fm Jay Moe amesema kuwa anaupenda sana wimbo wa Hakuna ‘Mungu kama wewe’ kati ya nyimbo za ijili zilizofanya vizuri Tanzania ulioimbwa na kwaya ya kijitonyama.

Hata hivyo Jay Moe alitoa heshima wa upande wa producer wa Bongo fleva  anayemkubali kuwa ni Mr. T Touch ambaye ndiye mtayarishaji wa kazi ya Jay Moe mpya.

“Bongo kwa sasa producer ambaye mi namkubali ni Mr t touch kutoka Touch sound, kwasababu  ndio one of the best producers kwa sasa ata ngoma ya Muziki ya Darassa siku nimeisikia nilimpigia simu na kumuambia nilivyoilewa beat” amesema Jay Moe.

Comments

comments

You may also like ...