Header

50 Cent ajiondoa kwenye tour ya Chris Brown dakika za mwisho

50 Cent amejiondoa kwenye ziara ya Chris Brown, The Party Tour katika dakika za mwisho. Amechukua hatua hiyo baada ya kushindwa kukubaliana kwenye malipo kati ya uongozi wa 50 na promota wa ziara hiyo.

Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa 50 alikuwa tayari kujiunga kwenye ziara hiyo baada ya mazungumzo ya kwanza na uongozi wa Chris ambao ulikubaliana kuhusu malipo.

Promota Live Nation iliamini kuwa 50 ameridhia na hivyo kumweka kwenye matangazo. Hata hivyo muda wa kusaini mkataba ulipofika 50 alikuta mpunga ulioandikwa haueleweki na hivyo kutosa, kwa mujibu wa TMZ.

Kulikuwa na mazungumzo ya kuweka sawa mambo lakini 50 aliwatolea nje wiki mbili zilizopita. Baadhi ya mashabiki sasa wamemind wakidai kuwa walinunua tiketi ili kumuona Fiddy.

Kupitia Instagram 50 ameandika:I would never say my friends can’t afford me. This run wasn’t handled correctly, I’m still on set filming Den of Thieves.

Ziara hiyo itaendelea kama kawaida leo huko Baltimore na mashabiki hawatarudishwa fedha zao kwasababu Chris atakuwepo kama kawaida.

Comments

comments

You may also like ...