Header

Alhaji Mzee Yusuf amuota Diamond Platnumz

Msanii nguli aliyestaafu muziki wa Taarabu Mzee Yusuf huwezi kumtupa nje ya mitandao yakijamii ingawaje ametangaza kuachana na muziki wa kidunia na kuamua kumtumikia Allah lakini bado humkosi mitandaoni.

Leo mapema alivamia kwenye ukurasa wa Instagram Diamond Platnumz na kuacha Comment ambayo ilisomeka kama ushauri wake alioupata akiwa kwenye jozi na ushauri huo ambao aliupata kwenye ndoto ulisomeka “Aslam aleykum kama ndugu yangu katika imaan leo nimekuota ukiwa unasoma QUR ANI tena kwa sauti nzuri sana naona si jambo la kulificha maana kwa nini nikuote ww sasa nakusihi usiache leo kusali ijumaa na sala nyengine labda Allah ana jambo jema kwako maana yy ndio muongowaji wa waja. Swali Allah akulipe mazuri zaidi ya hayo unayoyafikiria kichwani mwako. Mwenzyezi Mungu akutie nguvu na imani insha Allah. Amiin

Hata hivyo Mzee Yusuf amekazia kwa kujibu baadhi ya mashabiki wa Diamond Platnumz kuwa anamtakia kila la kheri kwenye muziki wake ila siku moja afikirie kuachana na mambo ya Kidunia na kurudi kumtumikia Allah kama yeye alivyojitolea.

Comments

comments

You may also like ...