Header

Baada ya Eric Shigongo kuliona Shimo la Diamond ‘Babu Tale’ atoka mapangoni na kumwaga povu

Baada ya Mjasiriamali Eric Shigongo kumtabiria msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz anguko kubwa la kimuziki kwa kile alichodai kuwa msanii huyo hafanyi show za kutosha nchini kutokana na Gharama kubwa anazochaji kwa matamasha ya ndani hatimae Meneja wake Babu Tale ametoka pangoni na kuikingia kifua timu nzima ya Uongozi wa WCB kwa kuweka mambo hadharani.

Babu Tale amechukuwa uamuzi wa kumjibu Eric Shigongo kwa choko choko zake alizozianzisha mapema wiki hili akidai kuwa shimo la kudondoka kwa Diamond Platnumz lipo karibu na sababu kubwa akitaja kuwa ni Mameneja wake.

Endelea…. Je, yule kijana wa Tandale, Temeke, Mbagala mwenye fulana kubwa iliyoandikwa WCB ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Jibu rahisi ni kwamba hatoweza.
Ni lazima afikirie ajue kwamba gharama anazotoza sehemu nyingine ziwe tofauti na Tanzania, au azifanyie gharama hizo kampuni kubwa za mitandao ya simu na vinywaji lakini si mtu binafsi.
Mara nyingi amekuwa akisema huko nje analipwa zaidi ya milioni mia moja, je, ni halali hata kwa Watanzania wenzake waliomfanya kuwa hapo alipo kuwatoza kiasi hicho cha fedha huku huyo anayemchukua akitarajia shoo yake iingiwe na watu wa hali ya chini wenye kiu ya kumuona?Labda Naseeb Abdul mwenyewe ndiye aliyelazimisha ada hii, kama si yeye bali ni mameneja wake (Salam na Tale) basi wanamshauri vibaya na matokeo yake kutofanya shoo nyumbani kwake (Tanzania) kutamfanya apoteze kupendwa na mashabiki sababu ya umbali alioutengeneza.Ikumbukwe kwamba watu hununua bidhaa ya mtu wanayempenda, mtu akichukiwa na bidhaa zake hususiwa.Diamond na WCB ni biashara ya Naseeb Abdul, hivyo basi Naseeb Abdul hatakiwi kuthamini sana fedha na kusahau mashabiki zake waliomfanya kuwa hapo alipo. Kifike kipindi awaeleze mameneja wake “HAPANA! TANZANIA NI NYUMBANI NA HAWA NI NDUGU ZANGU”Basi kama waandaaji watashindwa kumudu gharama zake sababu Naseeb ni mfanyabiashara kama mimi, basi afanye shoo ya kujitolea (Charity show) kama tuliyofanya naye huko Tandale huko Mwanza, Kigoma, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro kwenye viwanja kwa kiingilio cha shilingi 3000 na kisha fedha hizo azipeleke kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na hiyo itamfanya kupendwa na mashabiki na kumfanya kwenda juu kimuziki.TOFAUTI NA HAPA, MBELE YAKE KUNA SHIMO, UKIMYA WAKE BILA SHOO NYUMBANI UTAMZAMISHA!! MWISHO.“Ujumbe wa Eric Shigongo kwenda kwa WCB.

Baada ya ujumbe huo Babu Tale amesema chokochoko zote za Shigongo zimekuja baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kwenye show ya WCB iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Dar Live ambao unamilikiwa na Shigongo na kudai kuwa awali walielewana kwa asilia fulani ambayo baadae akaipandisha baada ya kuona mapokezi mazuri ya matangazo kutoka kwa wadau na kuongeza asilimia za tozo.

Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya…baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako… siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata…ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali…. tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu… Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie tume kaa kimya… na kujifanya unazunga eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?….. Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? …na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost… ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa….tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na amshabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe….mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa….yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum’bomoa msanii kupitia magazeti yako…..tafadhali heshimu heshima yetu kwako?” Ameandika Babu Tale.

Hata hivyo Babu Tale hakusita kutoa kilio chake kwa Rais Magufuli kupunguza kukaza kamba ili vijana waweze kupata kipato kwani mpaka vigogo wanalia “…… “Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao…..?“Ameandika Babu Tale.

 

Comments

comments

You may also like ...