Header

Kuelekea mchezo wa Yanga vs Azam FC: Juma Mwambusi ajitoa ufahamu

Kocha msaidizi wa Yanga SC, Juma Mwambusi amefunguka kuwa timu yake imebakiza mechi sita ngumu ili kutetea ubingwa hivyo anawaanda vijana wake waanze kwa kushinda mchezo wao na Azam FC utakaofanyika kesho katika dimba la Taifa.

Mwambusi amefunguka mbinu ambazo zitawapatia ushindi katika michezo hiyo yeye na kocha mkuu bwana George Lwandamina ambapo amesema kikubwa ni kutilia mkazo eneo la kiungo na safu ya ushambuliaji ili wawe na uwezo mkubwa kutengeneza nafasi na kuzitumia.

Kocha huyo msaidizi amesema kuwa katika kutetea ubingwa wao umakini mkubwa unahitajika hasa ikizingatiwa kuwa zipo timu ambazo zinapambana kuepuka kushuka daraja na nyingine zikitaka kutwaa ubingwa kitu ambacho ni changamoto kubwa kwa timu yao.

Hata hivyo Mwambusi amesema timu yake haiishi kwa historia, hivyo kichapo walichokipata kwenye Mapinduzi Cup hakiwafanyi kuwaogopa Azam katika mchezo wa kesho Jumamosi.

“Mchezo wa Jumamosi kwetu ni mpya na hatusumbuki na historia za nyuma . Hata ukikatika kidole unabakiwa na kovu baada ya kupona na siyo kidonda hivyo vijana wataingia uwanjani na dhana ya kusaka ushindi wa mechi hiyo siyo historia. Malengo yetu ni ubingwa sio kuwaza nyuma kilitokea nini” Alisema Mwambusi.

Comments

comments

You may also like ...