Header

Kuelekea mechi ya Yanga vs Azam FC: Simon Msuva aahidi furaha jangwani

Winga wa klabu ya Yanga na Timu ya taifa ametia neno kuelekea mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya klabu ya Azam FC unatarajiwa kupigwa Kesho kunako Dimba la Taifa.

Akizungumza na DizzimOnline Saimon Msuva amesema kla mchezaji yuko vizuri na kuahidi kuwa watapigana kwa hali na mali ili ushindi uweze kupatikana ili kujijhakikishia kubaki kwenye mbio za ubingwa wa Ligi.

“Kila mchezaji yupo vizuri na tuna uhakika kila mchezaji atapambana kwa nafasi yake ili kupata ushindi japokuwa naamini Azam ni Timu nzuri kwani wanashiriki hadi michuano ya kimataifa”Amesema Simon Msuva

Azam Fc watashuka Dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kuwaadhibu Yanga kwa kipigo cha Goli 4-0 Kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi.

Comments

comments

You may also like ...