Header

Michepuko yamponza Jose Chameleone

Staa wa ngoma ya ‘wale wale’ Joseph Mayanja a.k.a Jose Chameleone amemjia juu promota wa muziki kwa kusambaza maneno yanayoweza kumvunjia mahusiano yake na mkewe.

Taarifa awali zilizosambaa mitandaoni nchini Uganda zinadai kuwa promota Sipapa amehusika kusambaza taarifa hizo kwa kile alichodai kuwa Chameleone ametoka kimapenzi na mpenzi wake.

Hata hivyo Jose Chameleone amemfungulia Sipapa mashtaka kwa kosa na kumchafulia jina na kwasasa wawili hao hawawezi kupikwa chungu kimoja.

Vile vile Promota Sipapa amewahi kunukuliwa kuwa amejiribu hata kuwatumia watu wa karibu wa Chameleone ili wayamalize jitihada zilizogonga mwamba.

Comments

comments

You may also like ...