Header

Nuh Mziwanda ‘awazodoa’ mashabiki wake

Msanii wa wa bongo fleva anayetamba na ngoma ya anameremeta, Nuh Mziwanda amewataka mashabiki zake kutompangia jina la mtoto wake na kusisitiza yeye kama baba ndiye mwenye mamlaka hayo.

Kupitia kipindi cha eNewz ya EATV,  Nuh amefunguka kwamba hawezi kumuita binti yake majina ya kizungu kwa madai kuwa siku akikua na kwenda kwenye asili yake atakutana na hayo majina hivyo hakuna haja ya kumpatia mtoto majina yasiyo ya asili kwani hata mastaa wakubwa wana majina ya asili lakini wanaingiza pesa akimtolea mfano Iyanya na wengineo

“Mimi ndiyo baba wa mtoto ninatakiwa kujua jina la mtoto, nimempatia binti yangu jina la mama yangu mzazi ambaye kwa kifupi namuita Anya, hii ni damu yangu mimi kwa atakayeona jina halimpendezi ni yeye tu kwani sipangiwi cha kufanya kwenye maisha yangu binafsi lakini mimi najivunia na ninalipenda” – Alisema Nuh Mziwanda.

Comments

comments

You may also like ...