Header

Taarifa rasmi kuhusu afya ya Method Mwanjali kuelekea mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Kuelekea mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya klabu ya  Simba yenye makazi yake mitaa ya msimbazi-Kariakoo  jijini Dar es salaam  watamkosa beki wao tegemezi wa kati  Method Mwanjali  baada yakumia kwenye mchezo wao dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Akizungumza na DizzimOnline Makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange “Kaburu” amesema kuwa timu iko vizuri kwani vijana wana hari na wanania ya kupambana na kuhakikisha wanapata alama zote tatu kwenye mchezo dhidi ya Kagera.

“Method Mwanjali amebaki Dar es salaam kuendelea  na matibabu yake ili kupona kabisa ila vijana wengine wako tayari kupambana na kuakikisha wanapata alama tatu mbele ya kagera na kumaliza michezo yote mitatu  kanda ya ziwa kwa kuibuka na ushindi kwenye kila mchezo tunawashukuru mashabiki walivyotupokea hapa Bukoba” Alisema Kaburu .

 

Comments

comments

You may also like ...