Header

Barakah The Prince akiri udhaifu wake

Msanii na hitmaker wa ngoma ‘Acha niende’ aliyechini ya usimamizi wa menejimenti ya Rock Star 4000  amezungumzia madhaifu aliyonayo linapokuja suala ya kimawasiliano baina yake na watu wake wa karibu pia mashabiki.

Barakah amesema kuwa amegundua kuwa ni mtu wa hasira na lazima aje juu linapokuja jambo lisilomfurahisha na ni mwepesi ya kupigana bila kujali mazingira ingawa amebainisha kuwa amegundua tatizo lake na anahitahidi sana kujirekebisha.

 

“mimi ni mtu ambaye napanic sana lakini siku hizi najitahidi najicontrol…mimi ni mtu wa papo kwa papo mi ngumi mkononi lakini mpaka ifike hatua tunakabana sijui umenifanya nini” Alisema Barakah The Prince alipokuwa akizungumza na kipindi cha Ngaz kwa Ngaz.

Hata hivyo Barakah amekiri kuwa msanii ambaye amewahi kumjibu kwa kuwatukana baadhi ya mashabiki kutoka na kukerwa na baadhi ya maoni katika mitandao yake ya kijamii.

Comments

comments

You may also like ...