Header

‘Belle Nine na Diamond ndiyo wamenirudisha kwenye muziki’ – Saida Karoli..

Kama hukua unafahamu inabidi ufahamu kuwa Belle Nine na Diamond Platnumz ndiyo wasanii pekee ambao wamefanikiwa kumrudisha Saida Karoli kwenye ramani ya muziki baada ya kukata tamaa na amesema tayari alikua ameshaanza kurudisha vitu kijijini kwao.

Mahojiano yake na XXL ya Clouds FM,Saida Karoli amesema >>’Nilishatamani kuacha muziki na nilishawahi kuhamisha baadhi ya vitu vyangu kurudi kijijini na ndiyo kipindi hiko hiko Belle Nine na Diamond walitoa nyimbo ya Chambua kama karanga,wakanirudisha maana ilikua safari kabisa’

‘Maandalizi makubwa tu nilikua nimeshayafanya huko kijijini hii ni mara ya kwanza kukata tamaa kwa sababu siku zote huwa napambana nasema nitaimba muziki mpaka kufa kwangu lakini ilifika hatua nikasema hapa nimeelemewa kabisa’ – Saida Karoli.

Comments

comments

You may also like ...