Header

Haruna Niyonzima awapa somo viongozi wa Yanga

Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima huenda akawa tofauti kidogo na mawazo ya viongozi wa Klabu hiyo kwa kile anachoamini kuwa kuhama uwanja kwa kigezo cha kuwakimbia mashabiki sio tiba ya kupata matokeo mazuri.

Hivi karibuni Yanga iliwasilisha maombi shirikisho la soka Afrika CAF ili mechi yao ya nyumbani ya mchujo kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya kombe ka shirikisho barani Afrika ichezwe kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza badala ya uwanja wa taifa.

Maombi hayo hayakufanikiwa baada ya uwanja wa CCM Kirumba kutokidhi viwango vya CAF na kutakiwa kufanyiwa marekebisho ambayo hayawezi kukamilika ndani ya muda kabla ya mechi hiyo kitu ambacho Niyonzima kwake hakukitilia maanani na kusema ishu sio kuhama uwanja bali ni maandalizi kauli ambayo ni funzo tosha kwa Viongozi wa Yanga.

Ukijiandaa vizuri haijalishi uwanja, Mwanza sio mbali mashabiki wanasafiri hadi nje ya nchi sasa Mwanza watashindwaje kwenda kwa hiyo presha ambayo tunaipata hapa haitakuwa tofauti sana na ya Mwanza kwa sababu ni Tanzania ileile.”Alisema Niyonzima mbele ya Kamera za Azam TV.

Kwa upande wangu haina haja kubadili uwanja kwa sababu mpira unaweza kuchezeka sehemu yoyote. Sidhani hata kama walimu walipendekeza hivyo, itakuwa ni wadau lakini mpira wa kisasa hauko hivyo, sehemu yoyote unacheza mpira inategemea na wewe ulivyojiandaa.”Alisema Niyonzima.

Kwa maana hiyo Yanga itacheza mechi yake dhidi ya MC Algers kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam na si vinginevyo

Comments

comments

You may also like ...