Header

‘Mama yangu amelia baada ya kusikia nimetangaziwa vita na Shigongo’ -Babu Tale.

Babu Tale ni moja kati ya viongozi wa WCB ambaye toka wiki iliyopita ni kama ameingia kwenye mlolongo wa kurushiana maneno kati yake na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers Erick J Shigongo baada ya post ya Shigongo ikimtaka Diamond kuwa makini na watu watatu aliowataja ambao ni Babu Tale,Sallam na Nasib Abdul,hizi ni post alizoandika Shigongo.

MY CONFESSION Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo. Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha. Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania. Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO! LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE. Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti. Nitaendelea kesho.

A post shared by Eric Shigongo (@ericshigongo) on Mar 28, 2017 at 5:31am PDT

Jana dakika chache tu baada tu ya kuposti nilichokiandika juu ya Diamond Platnumz, Babu Tale, meneja wake, alinitumia ujumbe huo hapo juu, nafikiri kwa sababu ni mtani wangu; NAENDELEA… Wakati fulani nilikuwa nimeandaa tamasha la bure huko Tandale, eneo la watu maskini kabisa kwa lengo la kuwafundisha mbinu mbalimbali za kujiondoa katika umaskini, nilifanya hivyo nikiamini yako mambo ambayo watu waliofanikiwa huyafanya na watu wasio na mafanikio huyaepuka. Niliwaomba wasanii wengi sana waje kushirikiana nami katika tamasha hilo, wengi walikataa wakidai kiasi kikubwa cha fedha, waliokubali kuimba bure kwenye tamasha hilo ni R.O.M.A na Kala Jeremiah, nikiwa na idadi ya wasanii wawili tu na sitaki kutumia fedha kumlipa msanii kwenye jambo la kijamii kama hilo hatimaye niliamua kumpigia Diamond Platnumz ILI AJITOLEE NA TUFANYE KITU KWA AJILI YA JAMII. Naomba niseme wazi, nilikuwa najaribu maana ninajua kabisa gharama zake huwa ni kubwa, nimewahi kumlipa shilingi milioni thelathini kufanya shoo moja pale Dar Live, katika hali ya kushangaza kabisa, pamoja na umaarufu wake mkubwa Diamond ALIKUBALI KUFANYA SHOO ILE BURE! Wakati msanii kama Snura aligoma. Tukio hili lilinifanya NIMPENDE NASEEB ABDUL mara mbili zaidi ya ilivyokuwa hapo awali, ni MNYENYEKEVU, mtu wa kujishusha na asiyependa ugomvi na watu! Hakika kama mzazi ingawa sipendi sana mwanangu awe mwanamuziki, natamani kuwa na mtoto mwenye sifa hizi, sipendi majivuno, sipendi watu wanaoringa na kujiona wao ni bora kuliko wengine kwa sababu tu wana vitu fulani ambavyo wengine hawana. Mtu yeyote akipata nafasi ya kuongea na Diamond Platnumz amuulize ni mara ngapi nimekwishaongea naye na kumshauri juu ya uwekezaji wa fedha anazozipata leo, sababu MWANADAMU HUWEZI KUWA BINGWA MILELE, siku moja lazima tu utapigwa, jua huwa haliwaki siku zote, lazima usiku utaingia, umejiandaaje kwa ajili ya usiku au siku utakapopigwa ndiyo jambo la muhimu katika maisha haya. Endelea kuisoma picha hapo juu

A post shared by Eric Shigongo (@ericshigongo) on Mar 29, 2017 at 9:54am PDT

Endelea…. Je, yule kijana wa Tandale, Temeke, Mbagala mwenye fulana kubwa iliyoandikwa WCB ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Jibu rahisi ni kwamba hatoweza. Ni lazima afikirie ajue kwamba gharama anazotoza sehemu nyingine ziwe tofauti na Tanzania, au azifanyie gharama hizo kampuni kubwa za mitandao ya simu na vinywaji lakini si mtu binafsi. Mara nyingi amekuwa akisema huko nje analipwa zaidi ya milioni mia moja, je, ni halali hata kwa Watanzania wenzake waliomfanya kuwa hapo alipo kuwatoza kiasi hicho cha fedha huku huyo anayemchukua akitarajia shoo yake iingiwe na watu wa hali ya chini wenye kiu ya kumuona? Labda Naseeb Abdul mwenyewe ndiye aliyelazimisha ada hii, kama si yeye bali ni mameneja wake (Salam na Tale) basi wanamshauri vibaya na matokeo yake kutofanya shoo nyumbani kwake (Tanzania) kutamfanya apoteze kupendwa na mashabiki sababu ya umbali alioutengeneza. Ikumbukwe kwamba watu hununua bidhaa ya mtu wanayempenda, mtu akichukiwa na bidhaa zake hususiwa. Diamond na WCB ni biashara ya Naseeb Abdul, hivyo basi Naseeb Abdul hatakiwi kuthamini sana fedha na kusahau mashabiki zake waliomfanya kuwa hapo alipo. Kifike kipindi awaeleze mameneja wake “HAPANA! TANZANIA NI NYUMBANI NA HAWA NI NDUGU ZANGU” Basi kama waandaaji watashindwa kumudu gharama zake sababu Naseeb ni mfanyabiashara kama mimi, basi afanye shoo ya kujitolea (Charity show) kama tuliyofanya naye huko Tandale huko Mwanza, Kigoma, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro kwenye viwanja kwa kiingilio cha shilingi 3000 na kisha fedha hizo azipeleke kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na hiyo itamfanya kupendwa na mashabiki na kumfanya kwenda juu kimuziki. TOFAUTI NA HAPA, MBELE YAKE KUNA SHIMO, UKIMYA WAKE BILA SHOO NYUMBANI UTAMZAMISHA!! MWISHO.

A post shared by Eric Shigongo (@ericshigongo) on Mar 31, 2017 at 5:44am PDT

SASA NAMALIZIA MJADALA WA DIAMOND PLATNUMZ Kama nilivyosema wakati naanza kwamba ninampenda sana Diamond kwa sababu amekuwa mtu wa kujituma, aliyeng’ang’ania kutoka kwenye umasikini mpaka kuwa na mafanikio aliyokuwa nayo. Ieleweke kwamba sipo kwa ajili ya kumsema, kumponda, hapana, nipo kwa ajili ya kumshauri kama mdogo wangu, rafiki yangu kwa hiyo naomba nisieleweke vibaya. Diamond Platnumz kwao ni Tanzania, ni mwanamuziki wa Kitanzania na hata wapenzi wake wengi wanaomsapoti kwa nguvu nyingi ni Watanzania ambao asilimia kubwa vipato vyao ni vya chini mno. Wengi wanatamani kumuona akifanya shoo katika ardhi yake ya nyumbani, lakini badala yake wamekuwa wakimuona mara nyingi akifanya shoo Marekani, Ulaya, Nigeria, Afrika Kusini, kwenye Mashindano ya Afcon na sehemu nyingine nyingi ambazo ni nje ya Tanzania, mahali alipozaliwa na kuthaminiwa, mahali ambapo aliweza kujijazia mashabiki wengi. Mashabiki zake wanahitaji shoo, kumsoma kwamba amejenga nyumba, amenunua au amepata watoto na Zari si kitu ambacho mashabiki wanakihitaji zaidi kutoka kwake, wanachohitaji ni kuona shoo zake kwa wingi kama kilivyokuwa kipindi cha Moyo Wangu, Kamwambie na nyimbo nyingine. Ni kweli ana jina kubwa, ana mashabiki wengi, amepambana sana kufika alipokuwa lakini kwa upande mwingine anatakiwa kuangalia gharama za shoo zake hasa anapofanya nchini Tanzania, kwa watu ambao walimfanya leo kujulikana zaidi kama Diamond na si Naseeb Abdul. Leo, Diamond anafanya shoo kwa dola 55,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100. Hii inamaanisha kwamba kwa mtu kama mimi, nikimchukua Diamond kwa gharama hiyo inamaana kwamba nitataka niingize kiasi kikubwa kama faida, kwa hiyo badala ya kufanya shoo Dar Live, Diamond Jubilee au sehemu nyingine, nitaihamishia shoo yangu Mlimani City na kufanya kiingilio cha shilingi elfu hamsini. Swali la kujiuliza, je, yule bodaboda anayepiga sana nyimbo za Diamond ataweza kuingia kwa kiingilio cha shilingi elfu hamsini? Yule kijana anayatafuta riziki kwa kuingiza nyimbo za Diamond kwenye simu za wateja ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Je, yule kijana wa Tandale, Temeke, Mbagala mwenye fulana kubwa iliyoandikwa WCB ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Endelea nayo?

A post shared by Eric Shigongo (@ericshigongo) on Mar 31, 2017 at 5:40am PDT

Baada ya post hizo Meneja wa WCB ambaye ametajwa na Shigongo kuwa Diamond inabidi awe nao makini,Babu Tale kupitia akaunti yake ya Instagram nae alipost ya kumjibu Mkurugenzi huyu wa Global Publishers amesema.

Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya…baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako… siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata…ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali…. tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu… Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie tume kaa kimya… na kujifanya unazunga eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?….. Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? …na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost… ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa….tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na amshabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe….mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa….yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum’bomoa msanii kupitia magazeti yako…..tafadhali heshimu heshima yetu kwako?…… “Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao…..?”

A post shared by Hamisi Taletale (@babutale) on Mar 31, 2017 at 7:54am PDT

Baada ya hivi vyote kupita XXL ya Clouds FM imemtafuta Babu Tale kujua kiini cha matatizo au kurushiana maneno kwa yeye na Mkurugenzi wa Global ndg Shigongo ambapo Tale amesema..’Misunderstanding kubwa ni biashara tu labda yeye anafeel kuandika vitu,ana akaunti yake huwa anaandika watu’

‘Hajaanza leo kuandika biashara yangu vibaya kaanza kipindi magazeti yana nguvu sasa hivi hayana nguvu tena,hivi juzi iliongezeka speed baada ya kushindana kibiashara hatukufika pazuri ilikua tukafanye show Dar Live kitendo cha kuwa hatuwezi hatuwezi yakaja mengine’

‘Biashara ilikua inamhusisha Harmonize sio Diamond lakini Diamond ni msanii mkubwa,sina matatizo naye lakini ameshanambia atanionyesha kwenye vita mi nafata eneo langu la sheria lilivyo,nimeshawaambia familia yangu kuwa tatizo lolote litakalonitokea kuna mtu amenitamkia kwa mdomo wake nimeacha sauti yake kwao’

‘Mama yangu amelia wakati namwambia mimi kwetu last born halafu mimi ndo Gaucho nyumbani mimi ndo nipige mpira watu waende golini,mama yangu amelia nikamwambia usilie vitu vya kawaida hivi kwa Mwenyezi Mungu mambo yote yako sawa usijali mama’ -Babu Tale.

Comments

comments

You may also like ...