Header

Christian Bella atia neno kwenye bifu ya Ali Kiba na Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Christian Bella a.k.a King of  the best melodies anayefanya poa na kolabo yake ya Ollah aliyomshirikisha rapa kutoka Kenya Khaligraph Jones hazungumzia kinachoitwa bifu kati ya Ali kiba na Diamond Platnumz.

Bellah amesema kuwa anachojua ni kwamba wawili hao wanapendana sana na anaamini kinachoendelea baina yao ni ushindani tu na sio vinginevyo.

“sidhani kama wao wenyewe wana bifu, unajua  pia mashabiki wanapenda sana kukuza vitu sana……Ali Kiba na Diamond wakiwa wanashindana ni vizuri kimuziki…ukiniambia kwamba niwapatanishe naona kama haina sababu ya kuwapatanisha sidhani kama wanachukiana…ukiwaweka sehemu moja wataongea tu lakini watu wanakuza mambo” Alisema Christian Bellah alipokuwa akizungumza na Ayo Tv.

Hata hivyo Christian Bellah amebainisha shukrani zake kwa watanzania kwa support wanayompa kwenye muziki wake kiasi cha kujulikana zaidi Tanzania kuliko Kongo ambako ndo chimbuko lake.

Comments

comments

You may also like ...