Header

Jay Moe atimiza ndoto za Mr T. Touch

Rapa na hitmaker wa ngoma ‘Nisaidie kushare’ Juma Mchopanga a.k.a Jay Moe amezungumzia hali ya ugumu na urahisi wa upatikanaji wa mashairi kila anapo hitaji kuandaa wimbo na kusema kuwa mara nyingi ideas za nyimbo zake anazipata akiwa nje ya miji wa Dar es salaam na hajawahi kujua ni kwanini.

Akiuzungumzia wimbo wake mpya wa Nisaidie kushare Jay Moe amesema kuwa Mr. T touch alikuwa na ndoto kubwa za kufanye naye kazi ilikuwa kazi rahisi.

“Touch yeye alikuwa na dream ya kufanya kazi na mimi, kwa hiyo siku ambayo nilimpigia simu kwasababu nisaidie kushare demo alitengeneza Daz Knowledge…kwa hiyo Touch aliisikia ile demo…alichofanya yeye ni kutengeneza beat kama nne nikachagua moja nikaweka mashairi kazi ikaisha” Alisema Jay Moe alipokuwa akizungumza na Ayo Tv.

Hata hivyo Jay Moe amemiminia sifa na kum pongeza kwa uwezo wa kikubwa anachofanya kwenye muziki kwasasa.

Comments

comments

You may also like ...