Header

‘Natamani siku moja kuwa kama Bakhresa au Mo Dewji’ – Jokate

Inashauriwa muda mwingine mtu kuwa na  ndoto kubwa katika maisha ili zikusaidie kukutia moyo na kuhangaika kuipambania ili pengine hata ukishindwa kuifikia kwa asilimia mia moja ikusaidie hata nusu ya ndoto hiyo,kitu ambacho Jokate nae ameanza kukiota na kutamani kukifikia ni kuwa kwenye list ya matajiri wakubwa Tanzania na Afrika ambao ni Mo Dewji na Bakheresa.

Kwenye maneno yake aliyoyatoa baada ya kukabidhiwa tuzo ya Malkia wa nguvu amesema vitu anavyotamani ni siku moja kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa Tanzania na Afrika>>’Natamani siku moja kuwa kama Bakhresa niwe kama Mo Dewji,kwanini ni wanaume tu ndo wawe brands kubwa hapa nyumbani Tanzania wanatumia rasilimali hizi hizi na wanatuhudumia sisi pia’

‘Ndoto yangu ili iweze kufanikiwa nadhani inahitaji sapoti kuwa toka serikali,ituangalie sisi ambao tuna brands zenye sifa sana nadhani ukienda sehemu mbalimbali za Tanzania watu wanajua jina Kidoti lakini ule uwezo wa ku-transform jina likawa biashara kubwa tunahitaji sapoti ya serikali,ituangalie itubebe,mi nikiangalia kuna watu wanapenda brand yangu kutoka kenya,Rwanda lakini nazifikiaje hizo nchi’. -Jokate.

Comments

comments

You may also like ...