Header

Jonas Mkude awapigia magoti wanamsimbazi

Nahodha wa Klabu ya Simba Jonas Mkude amewatuliza mashabiki wa Simba kwa kuwafariji kuwa bado klabu yake inapambana kuhakikisha ubingwa wa msimu huu unatua msimbazi inawaje wamepoteza mbele ya Kagera kwenye Dimba la Kaitaba.

Mkude amesema mpaka sasa bado hawajakata tamaa kutwaa ubingwa kwani mechi bado zipo na kuwahakikishia mashabiki kuwa watatwaa ubingwa cha msingi ni kutoa sapoti kwenye timu yao kwa michezo iliyosalia.

Ndiyo matokeo ya mchezo japo tumepoteza lakini hatujakata tamaa tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunashinda ubingwa wa Ligi kuu kwani nafasi bado ipo,Na sasa tunajipanga kwa ajili ya michezo inayokuja ila nawaomba mashabiki wetu wasife moyo“Alisema Jonas Mkude.

Baada ya Simba kujeruhiwa na Kagera Sugar wataelekea Jijini Mwanza kuvaana na Toto Africa na Mbao FC.

 

Comments

comments

You may also like ...