Header

Nay wa Mitego atangaza hali ya hatari

Rapa Nay wa Mitego ametangaza hali isiyo kuwa ya kawaida hususani juu usalama wa maisha yake kwa kile alichosema kuwa anaviziwa auwawe na watu wasiojulikana huku chanzo kikiwa bado hajakiweka wazi moja kwa moja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego ametangaza hali hiyo ya hatari kwa kuandika “Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa, Wana panga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod

Nay wa Mitego wiki mbili zilizopita alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma ambazo hazikuwekwa wazi lakini baadae aliachiwa na Jeshi la polisi kwa amri ya waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe na baadae kuitwa kwa mashauriano na Waziri Mwakyembe yaliyokuwa na lengo la Kuboresha mashairi ya wimbo wake wa ‘WAPO’.

Comments

comments

You may also like ...