Header

The UnderTaker aachana na mieleka

Hakuna marefu yasiyo na ncha!!Jana usiku ulikuwa ni usiku ambao kwa mashabiki wa mchezo wa mieleka hawawezi kuusahau kwani kulikuwa na mechi za Wrestlemania kwa mapambano mawili yaliyokuwa yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu ambapo Goldberg alivaana na Brock Lesnar huku mpambano mwingine mkali na wakukata na shoka ulikuwa ni wa The Undertaker na Roman Reigns.

Mapambano hayo mawili yalivuta hisia za watu wengi duniani wakitaka kumjua nani mbabe kati ya hawa,Na kwenye mechi kati ya Lesnar na Goldberg, yalitokea matokeo ambayo watu wengi hawakuyapenda wala kuyatarajia Brock Lesnar alimpiga Goldberg na kuchukua mkanda wa Universal Champion.

Pambano ambalo lilikuwa kubwa zaidi lilikuwa kati ya Roman Reigns na Undertaker,Kwa muda mrefu hili lilikuwa likizungumziwa kutokana na ubora wa Reigns wengi wakiuliza atafanya nini kwa mbabe wa KO Under Taker.

Image result for Roman Reigns na Undertaker

Roman Reigns jukwaani na Under Taker akiwa nje ya ulingo.

Reigns ambaye alionekana kummudu Under Taker japo kuna muda naye alielemewa na kuonekana kama atapoteza mchezo huo lakini akashinda mbabe huyo na muda mfupi Baada ya mchezo huo Undertaker alivua kofia, gloves na koti lake kuashiria ni mwisho wake kupanda ulingoni na kisha akaondoka na kuwaacha mashabiki wengi wakibubujikwa na machozi.

Mark William Calaway maarufu kama Under Taker ni mmoja kati ya wanamieleka bora kuwahi kutokea katika WWE akiwa ameshawahi kubeba karibia mikanda yote ya mchezo huo, huku pambano lake la kwanza ikiwa mwaka 1984 miaka 33 iliyopita.

Kupitia kurasa zao za twitter wana mieleka wengi na mashabiki wa mchezo huo duniani walionesha hisia zao na kumshukuru Under Taker kwa kazi kubwa aliyofanya kipindi chote akiwa ulingoni na kwa upande mwingine jana tulishuhudia Mwanamieleka mwingine John Ciena akimvisha pete ya uchumba mrembo Nikki Bella.

Comments

comments

You may also like ...