Header

Mdogo wake Mez B kuja na kitabu kinachozungumzia maisha ya Chamber Squad

Kama ukiambiwa utaje makundi 3 bora yaliyowahi kutokea Tanzania kwenye muziki wa kizazi kipya huwezi kuacha kulitaja kundi la Chamber Squad ambalo ndani yake lilikua na wasanii wakali kama Marehemu Ngwair,Marehemu Mez B,Nourah na Dark Master.

One six ni mdogo wa Mez B ambaye Nourah aliwahi kumtambulisha kama Mwanachemba mpya na mdogo wake Mez B huyo kwa sasa amekuja Dar kwa ajili ya mkakati wa kutoa kitabu kitakachohusu maisha ya wasanii wa Chamber Squad na mwenendo mzima wa kundi hilo kwa sasa.

XXL ya Clouds FM imeongea na One Six na amesema>’Niko Dar kwa ajili ya project zangu lakini kwa ajili ya luandaa kitabu cha Chamber Squad kitu ambacho kimekua historia,haiwezekani ndani ya miaka 2-3 wakafa watu wa kundi moja mfululizo hii inamaanisha kuna jambo’

‘Tumekaa na kufikiria tukaona tutoe kitabu chenye historia kwa sababu hawa watu walikaa wakaaminiwa toka siku ya kwanza pia ni miongoni mwa waanzilishi wa Bongo fleva Tanzania ikawakubali na kuamini hawa ndiyo wenye dhamana ya muziki wa Tanzania’. -One six.

 

Comments

comments

You may also like ...