Header

‘Muziki tulioutengeneza na Davido sio muziki wa kupitwa na wakati’-Joh Makini.

Davido na Joh Makini kwa sasa wako South Africa na kubwa zaidi lililowapeleka huko ni kutengeneza video ya wimbo wa Joh Makini ambao ndani yake kamshirikisha Davido,wimbo ambao kihistoria ya nyimbo zilizorekodiwa kipindi cha nyuma bila kuachiwa rasmi inaingia kwenye list hiyo.

kupitia Snapchat ya Davido na instagram ya Davido alithibitisha utokaji wa kolabo hiyo ambayo maneno yalianza kuwa mengi zaidi,Joh Makini amehojiwa na XXL ya Clouds FM na amesema>’Huu wimbo haukutoka mapema zaidi kwa sababu tulipourekodi hatukupanga utoke haraka kiasi hicho’

‘Muziki ambao tumeutengeneza na Davido sio muziki wa kupitwa na wakati hakuna mtu alikua na stress suala la huu wimbo kuwa ndani,kwa sababu mimi nimeendelea na kazi zangu na ngoma nyingi kali zimetoka baada ya huu wimbo na hakuna kitu kimeharibika na Weusi wako juu’

‘Davido ndiye aliyenicheki juzi kati kwamba sasa mwanangu time imefika tukutane South Africa tufanye video ya huu wimbo,hivyo nikasafiri kutoka Bongo tukakutana South Africa,watu wasiwe na haraka tuwe na moyo wa subira,nina ngoma nyingi sana nimefanya na wasanii wa nje zipo ndani tu’. -Joh Makini.

Comments

comments

You may also like ...