Header

Fahamu mengi juu ya ujio mpya wa Belle 9 na Saida Karoli

Msanii wa bongo fleva na hitmaker wa ‘Give it to me’ Belle 9 ameuzungumzia kwa undani ujio wa kazi yake na Saida Karoli ngoma iliyorecordiwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Akizungumza na Dizzim Online Belle 9 amesema kuwa uongozi wake ulifanya jitihada za kumtafuta Saida kwa lengo la kufanya kazi ya pamoja na kazi imekamilika tayari chini ya studio za B Records kwa ushirikiano wa watayarishaji Chizan Brain na Buggahleez.

Belle 9 na Saida wakiwa studio

“kama movie siku moja tukakutana tu studio siku ambayo hatukuwa tumearrange basi kama unavyojua mkishakutana studio alikuwa na session yake pale kuna wimbo alikuwa anatakiwa kuurecord na mimi nikaanza kupata mzuka pale basi nikafanya ambacho nimekifanya na ngoma ni kubwa kiukweli” Alisema Belle 9.

Akizungumzia heshimaya Saida ‘Belle9’ ameongeza kwa kusema kuwa yuko tayari kufanya chohote kuhakikisha Saida anafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika muziki zaidi ya mafanikio yake ya awali.

Vile vile Belle 9 amebainisha kuwa utaratibu wa kukamilika kwa video uko kwenye mikono ya uongozi na muda wa kila kitu kwenda kwa mashabiki ukifika kazi itatoka.

Hata hivyo leo ni siku ya kumbukumbu ya tarehe ya kuzaliwa Saida Karoli  na Belle 9 ni moja ya wasanii waliomtakia maisha marefu.

 

Comments

comments

You may also like ...