Header

Kylie na Tyga waachana kwa mara nyingine

Tyga na Kylie Jenner wameachana kwa mara nyingine tena. Vyanzo vimethibitisha kuachana kwao kupitia tovuti ya People. “They tend to take little breaks all the time and then get back together. It’s definitely possible they’ll work things out again,” kilisema chanzo kimoja ambacho kinaamini watarudiana tena.

Tyga, 27 na Jenner, 19, wamekuwa kwenye uhusiano wenye matatizo kibao tangu mwaka 2014. Wameshawahi kuachana mara kibao nyuma ikiwemo mwaka 2015 baada ya kaka yake Kylie, Rob Kardashian kuanzisha uhusiano na Blac Chyna, ex wa Tyga. Mwaka jana waliachana pia.

Kuachana kwao awamu hii kumefuatia tuhuma za hivi karibuni za Blac Chyna dhidi ya Tyga kuwa ameshindwa kumhudumia mtoto wao na kumlipa msichana anayemwangalia.

Comments

comments

You may also like ...