Header

Matumizi ya kiingereza sio kigezo cha msanii kwenda kimataifa – ‘Wakazi’

Rapa kutoka Tanzania anyefanya vizuri na ngoma yake inayokwenda kwa jina ‘Tanganyika’ amezungumzia mahusiano yaliyopo kati msanii kwenda kimataifa na matumizi ya kiingereza katika muziki wa msanii.

Akizungumza na Dizzim Online wakazi amesema kuwa kumekuwa na fikra kwa baadhi ya wasanii, wadau na washikadau wa muziki kuwa matumizi ya lugha ya kiinegereza katika muziki jni njia ya kuupeleka muziki kimataifa jambo ambalo hakukubaliano nalo.

“kila msanii anasema anapigani kwenda kimataifa, watu wengi wanafikiri kwenda kimataifa ni suala tu la kuimba kiingereza mimi sikubaliani nalo…ukiimba kiingereza unaweza ukasikika au ukaeleweka kiurahisi lakini ukitoa muziki mzuri regardless umeimba kwa lugha gani kwasababu muziki ni zaidi ya maneno, ni ala za muziki, preparation na production quality… unaweza kutoka kimaifa pia na utofauti pia na utofauti wa muziki wako kwasababu ukiwapelekea kitu cha tofauti na yenyewe ni kutoka kimaifa” Amesema Wakazi.

Vile vile Wakazi ametuma shukrani za kutosha kwa vituo vya kimataifa vinayoendelea akuonesha kumkubali kama rapa kutoka Tanzania baada ya MTV Base East majuzi kumtaja kama mfalme wa rap kati ya wafalme wa muziki wa rap anayestahili kuheshimiwa kutoka Tanzania.

Comments

comments

You may also like ...