Header

Nay wa Mitego awatoa machozi wabunge mbele ya Kikwete

Wakati vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania vikiendelea leo Bungeni mjini Dodoma Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Kikwete ni moja ya watu waliohudhuria kama wageni kwenye kikao hicho.

Kitu kikubwa kwenye vikao hivyo ilikuwa ni pale alipokaribishwa Mh Kikwete na ukumbi wote wa Bunge kuanza kupiga makelele huku wengine wakishangilia kwa furaha huku Spika wa Bunge Job Ndugai akiingizia vipande vya wimbo wa Nay wa Mitego wa ‘WAPO’ .

Mh Ndugai alianza kwa kumkaribisha Kiketwe na ndiyo kelele za Wabunge zikisema tumekumiss na baadae Ndugai kuingizia mistari ya Nay wa Mitego kwa kusema  “Inaonesha hata waliom’miss nao Wapo“.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri walionekana kutokwa na machozi ya furaha baada ya kumuona Kikwete na hii inadhihirisha kuwa huenda alichokiimba Nay wa Mitego kwenye wimbo wake wa WAPO kimewagusa watu wengi sana kwenye Jamii.

Comments

comments

You may also like ...