Header

Ndoto za shule zamtesa Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Rap anayefanya vizuri na ngoma Kidebe anayefanya kazi chini ya usimamizi wa Tip Top Connection Dogo jana amezungumzia majuto yake ya kuwa nje ya maisha ya shule.

Akizungumzia majuto hayo Dogo Janja amesema kuwa anamiss sana maisha ya kuwahi kuamka kwenda shule na mpango wa kurudi upa ingawa sio karibuni kutokana na majukumu aliyonayo kwasasa.

“natamani siku moja nirudi shule niwe mwanafunzi kama kawaida kwasababu ni kitu ambacho uwa kinaniumiza sana kila siku nimekuwa nikikiwaza nikiamka namiss zile moments yaani kwamba naamka asubuhi na mimi najiandaa nawahi…kurudi shule ni vitu ambavyo vipo na vipo kwenye plan lakini sio kwasasa kwasababu kuna vitu ambavyo pia vinaigiliana, ukitaka usome akili inahitaji kuwa imerelax” Alisema Dogo Janja alipokuwa akizungumza na Ayo Tv.

Hata Dogo Janja sio mara yake ya kwanza kutamani kurudi shule tangu aliposhindwa kuendelea na masomo hata kutangaza kuchukua masomo ya Teknologia (IT).

Comments

comments

You may also like ...