Header

Simba yajichimbia Migodini,Geita

Baada ya wekundu wa Msimbazi Simba kuambulia kichapo mbele ya Kagera sasa yaelekeza nguvu zake kwa Toto Afrika na Mbao FC zote za Mwanza kwenye michezo yamuendelezo wa ligi kuu Tanzania Bara na Simba inaitajika kushinda michezo hiyo ili kurudisha matumaini ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Chanzo kutoka ndani ya klabu ya Simba kimeiambia DizzimOnline kuwa wameamua kufanya mambo yao kimya kimya ili kujiandaa na michezo hiyo migumu inayoikabili siku za usoni na wameamua kupigana kuhakikisha wanapata ushindi kwenye michezo hiyo.

Kwa sasa tumeamua kuelekeza nguvu zote kwenye mechi zilizobaki huku kanda ya ziwa na kuakikisha tunapata matokeo mazuri na ndio sababu yakufanya mambo yetu kimya kimyakwani tunaitaji kurejea kileleni mwa ligi kuu“Kilisema chanzo chetu.

Simba ambayo kwa sasa imeweka kambi Geita kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbao FC utakaopigwa wikiendi hii kwenye dimba la CCM kirumba jijini Mwanza.

 

Comments

comments

You may also like ...