Header

Enrique Iglesias aweka rekodi mpya soma hapa

Hakuna kitu kizuri Duniani kama kuona kazi yako inafanya vizuri hususani kwa wasanii wa Muziki na hili linadhihirika kwa mkongwe Enrique Iglesias ambae nae ameingia kwenye orodha ya wasanii waliotazamwa zaidi Youtube.

Wimbo wa Enrique Iglesias ‘Bailando’ aliowashirikisha Descemer Bueno na Gente De Zona umefanikiwa kutazamwa mara bilioni 2 kwenye mtandao wa Vevo Wimbo huo wa Kilatin ulitoka mwaka 2014.

August 2015, ilipata views zake za kwanza bilioni moja na kuwa wimbo wa kwanza wenye lugha ya Spanish kufikia namba hizo Muimbaji huyo hakusita kufurahia mafanikio hayo kwa kuandika kwenye Instagram, “Thank you to all my fans! I love you guys!”

Comments

comments

You may also like ...