Header

Msami amtolea uvivu AT

Dancer maarufu na Msanii wa Bongo Fleva Msami amemchana AT na kumtaka aboreshe kazi zake badala ya kulalamika kuwa kuna watu wanaobebwa huku akimuonya kwamba wasanii anaowaita wacheza shoo wana maisha mazuri na mafanikio makubwa kumzidi yeye.

Msami ameonesha kukerwa na kauli ya AT iliyodai kuwa wanaobebwa kwenye muziki ni wale wanao ‘dance’ huku wakiwa hawajui kuimba,Katika hatua nyingine msanii huyo ameongeza kwamba AT hana ubora wowote kikazi ndiyo maana hawezi kuleta changamoto na wala hajawahi kufikiria kufanya naye kazi, huku akimkumbusha kuwa hao anaowaita wacheza show huwa anawatafuta kipindi anapokuwa anawahitaji kikazi.

“AT anaongea tu sababu hao dancers anaowasema yeye wana maisha nazuri kuliko yeye, wana fanbase  kubwa na wanafanya maendeleo kibao kwa kutumia vipaji vyao. Lakini cha ajabu sisi ambao ni madancers watu wanapenda muziki wetu na tukipanda stejini watu wana enjoy, kwa kuwa unawaimbia na bado unawaburudisha . Lakini hapo hapo bado alikuwa ananipigiaga simu nimtafutie wacheza show akiwa na kazi” Alisema Msami kwenye kipindi cha eNEWS cha EATV.

Msami ameonesha kukerwa na kauli ya AT iliyodai kuwa wanaobebwa kwenye muziki ni wale wanao ‘dance’ huku wakiwa hawajui kuimba kauli aliyoitoa kwenye mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio.

Comments

comments

You may also like ...