Header

Suge Knight atetewa juu ya kifo cha TuPac Shakur

Ni miaka 21 mpaka sasa tangu kufariki kwa rapa Tu Pac na kumekuwa na kesi inayomkabili producer na mmiliki wa Record Lebo ya Death Row Records Suge Knight kuhusu kuhusika kwenye kosa la mauaji tofauti kifungo alichoanza kukitumika mwaka 2015.

Kumekuwa na tetesi na taarifa zisizo rasmi kuhusu Suge Knight kuhusika katika kifo cha Tu Pac taarifa ambazo mtoto wa Suge mapema aleo kupitia ukurasa wa Instagram alikanusha na kusema kuwa baba yake hakuhusika na alikuwa mtu wa karibu sana na Tu Pac.

“Baba yangu alikuwa ni mtu mwenye kumlinda sana Pac. kama angajua kuwa kuna watu wanamtafuta isinge wezekana wawe pamoja katika kipindi cha muda mrefu. hizi tetesi zina ubinafi ndani yake na sioni umuhimu wake. Ukiangalia anayesambaza tetesi hizi hana nia njema na familia yangu na haijali kabisa.

Habari za kutengeneza hazitapata nguvu lakini watu wataacha kujarobu kutengeneza pesa kutoka kwenye familia yangu, hasa hasa kutokana na uongo. Ni habari hasi pekee zisizo nzuri kuhusu watu weusi zinapata kutangazwa ninavyoona.

BABA YANGU ANAHITAJI FAMILIA YAKE NA HAKI ZAKEHATA KABLA YA KUZUNGUMZIA HIZO MAKALA.

#FreeSuge ♦ Alipost Suge Knight.

 

 

Comments

comments

You may also like ...