Header

Abdi Banda ampigia magoti George Kavila

Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba maarufu kama wekundu wa Msimbaz Abdi Banda amemuomba radhi nahodha wa Kagera Sugar George Kavila kwa kitendo cha kumpiga ngumi katika pambano la Ligi kuu Tanzania Bara wakati timu zao zilipokutana Jumapili uwanja wa Kaitaba.

Banda ameiambia DizzimOnline hakukusudia kufanya tukio lile hivyo anamwomba msamaha nahodha huyo pamoja na wadau wote wa soka nchini kwani anatambua akufanya kitendo cha kisoka

“Nichukue nafasi hii kumwomba radhi Kavila najua haikuwa kusudio lango ispokuwa ilitokea katika harakati za kupigania jahazi la timu yangu kwani hata baada ya mchezo kumalizika nilimuomba radhi kwa kitendo nilichokifanya,”Alisema Banda

Baada ya kunusurika kadi Jumapili sasa Banda atalazimika kuomba dua na Kamati ya Saa 72 pia isimchukulie hatua kwa kitendo alichokifanya

Comments

comments

You may also like ...