Header

Baada ya Mnyama kuuwawa na Kagera Sugar; Mbao FC yaahidi kumzika

Timu ya soka ya Mbao FC ya Jijini Mwanza imeionya Klabu ya Simba kwamba haitakubali kufungwa kwenye mchezo ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi yao unaotarajiwa kuchezwa Jumatatu ya wiki lijalo.

Simba inatarajia kuwa mgeni wa Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jumatatu katika mechi ya Ligi Kuu bara ikiwa ni baada ya kupoteza mechi dhidi ya Kagera Sugar mwishoni mwa wiki iliyopita kwa mabao 2-1.

Ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kuongoza msimamo wa ligi na kujisafishia njia ya ubingwa Simba ilijikuta ikiangukia pua na kupata kipigo hicho kwenye uwanja wa Kaitaba,Mjini Bukoba na hivyo kutoa nafasi kwa Yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja ikiwa na pointi 56.

Kocha msaidizi wa Mbao FC, Soud Slim alisema wamekiandaa kikosi chao vya kutosha na Simba wasitarajie kuwafanya daraja katika mechi hiyo, kwani nao wamejiandaa kushinda na wana uhakika huo.

Mimi naomba wadau na wapenzi wa timu yetu waendelee kutuunga mkono pamoja na chama chetu cha soka Mwanza kitupe sapoti ili tumalize ligi katika nafasi za juu,” alisema Kocha msaidizi wa Klabu ya Mbao FC Soud Slim kwenye mahojiano yake na Gazeti la Habari Leo.

Comments

comments

You may also like ...