Header

Bahati yamuangukia Cassper Nyovest

Rapa kutoka Afrika ya Kusini na hitmaker wa ngoma Doc Shebeleza anayefanya vizuri na ngoma yake mpya Tito Mboweni ‘Refiloe Maele Phoolo’ a.k.a Cassper Nyovest aruka na dili kali na kampuni kubwa ya kinywaji.

Kupitia kurasa rasmi za Instagram ya kampuni hiyo ya kinywaji ya Ciroc ya Afrika Kusini na ya rapa ‘Cassper’ wamethibitisha kuwa Cassper Nyovest amekuwa balozi ambapo kila tukio linalo mhusu Cassper litakuwa linawekwa kwenye kila jukwaa la Ciroc kwa muda wa mwaka mzima.

“ni furaha kubwa sana kwangu kuwa miongoni mwa wanafamilia wa Ciroc. Sote tunajua kuwa nimekuwa nikitamani sana kukaa namba 1 hivyo kushirikiana na kinywaji namba moja cha gharama cha Vodka, ambacho siku zote kinahusu kusherekea mafanikio, nimekuwa nzuri sana kwangu. Naamini katika kusherehekea maisha kila wakati na nitawaleta Ciroc pamoja mashabiki wangu pamoja katika safari yangu na kuwapatia kila kinachoendelea kwa mwaka mzima. Mashabiki mnahitaji ona hii – tunayo mengi ndani” Alicomment Cassper.

Hata hivyo Cassper mwenyewe kupitia ukurasa wao aliwapongeza kuwa na kampuni hiyo kibiashara ambapo kampuni haikusita kuandika kupitia ukurasa wao wa Instagram “tumakulipa kwa cheque na @Casspernyovest ametua tena. tunakukaribisha katika familia ya Ciroc.” kwa maana ya kumkaribisha tayari kwa biashara.”

Hata hivyo sio mara ya kwanz kwa Cassper kudaka dili kubwa ambapo alishapata kuwa balozi ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya MTN ya Afrika Kusini mwaka 2015.

 

Comments

comments

You may also like ...