Header

Mashabiki wammind Lil Wayne kwa kuwachomesha mahindi kwenye show

AUSTIN, TX - MARCH 16: Lil Wayne performing at Stubbs during SXSW on March 16, 2017 in Austin, Texas. (Photo by Merrick Ales/WireImage)

Bosi wa Young Money, Lil Wayne amewakera mashabiki katika chuo kikuu cha Florida baada ya kupanda jukwaani kwa kuchelewa kwenye show yake ya Jumanne, April 4.

Rapper huyo hakupanda jukwaani kwenye ukumbi wa O’Connell Center hadi saa tano na dakika 26 usiku na kujikuta akizomewa alipopanda kutumbuiza kwakuwa show ilitakiwa kumalizika saa tano kamili.

Milango ilikuwa wazi kuanzia saa moja na robo na wasanii wa utangulizi walimaza kutumbuiza saa nne kamili za usiku. Zaidi ya watu 3000 walibaki wakisubiri kwa saa nzima kumuona Weezy akipanda jukwaani.

Hata hivyo uongozi wa O’Connell Center ulitangaza kuwa ndege ya Lil Wayne ilikataliwa kuruka kutoka Atlanta kutokana na kuwepo upepo mkali.

Comments

comments

You may also like ...