Header

Morocco Omari wa ‘Empire’ atiwa mbaroni

Muigizaji na mzaliwa wa Chicago Mr. Morocco Omari aliyepata umaarufu kupitia series ya Empire anayecheza nafasi kama mdogo wa Lucious amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kosa la kujihusisha na ugomvi.

Ugomvi unaomhusu Morocco Omari uliripotiwa na mwanamke mmoja aliyepiga simu polisi kupitia number 911 ya Chicago siku ya jumatano na nakutoa malalamiko kuwa amekuwa kwenye mabishano na Omari na amesukumwa mara kadhaa na kudai kuwa amepata maumivu kifuani na shingoni.

Taarifa hiyo iliyowapelekea polisi kufika eneo la tukio muda mfupi baadae mida ya saa nane na nusu mchana na kumtia mbaroni kwa kosa la kumdharirisha na kumdharau mwanamke yule.

 

Chanzo: TMZ

Comments

comments

You may also like ...