Header

Dayna akubali kuzungumzia kinachosemwa kuhusu Daxx Cruz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Komela’ aliomshirikisha Bill Nas, na mwanamitindo Daxx Cruz ni siku sio nyingi kumekuwa na mionekano tofauti ya hapa na pale kwenye picha ambazo zinaweza kutumika kuwaweka katika idadi ya watu wanaotoka kimapenzi.

Daxx Cruz

Akizizungumzia picha na nyakati zote anazoonekana na Daxx Cruz, Dayna Nyange amesema kuwa wao ni marafiki tu wa karibu tu tofauti na watu wanavyodhania kuwa  ni wapenzi na kuongeza kuwa ana mpenzi ambaye hakuwa tayari kumtaja.

“Daxx ni rafiki yangu tu…he is just a friend ila ni mtu ambaye tumeshibana lakini hakuna kwamba tuna mahusiano kaa watu ambavyo wanafikiria. Nimekuwa nikiongea  hivyo lakini sijui kwanini watu wanakuwa hawataki kuamini wengine wakija kutuona karibu ndo wanaamini…mkiniona nadeka kwa marafiki zangu kawaida japo nina mipaka” Alisema Dyana Nyange alipokuwa akiongea na E-News ya Ea Tv.

Hata hivyo Dayna amekuwa ni miongoni mwa wasanii wa siri sana hasa linapokuja suala la kuwa katika mahusiano kitendo kianchowapa wasi wasi baadhi ya wadau na mashabiki wenye uchu wa kujua maisha ya kiamahusano ya Dayna kuwa kwa wanachokiona pengine Dayna ameshindwa kujizui na ndo maana kinatokea wanachokiona.

 

 

Comments

comments

You may also like ...