Header

‘Tuzo imenifanya nijione nimekua kwa kiasi fulani’ – Dayna Nyange

Mwezi wa 4 ni mwezi ambao umekua mzuri kwa Dayna Nyange baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo za Bae zilizofanyika Nigeria tena akiwa Mtanzania pekee aliyeshinda kwenye vipengele viwili BEST AFRICAN ACT na Kipengele kingine alichoshinda ni Best Vocal Perfomance Female kupitia wimbo wake ‘Angejua’.

Wasanii wengi huongeza zaidi bei ya show na baadhi ya vitu vyao baada ya kuwa washindi kwenye tuzo mbalimbali hasa zinazokua za nje ya nchi (International Awards) swali hili alipoulizwa Dayna amesema kuwa kwake yeye ni tofauti>’Tuzo ina heshima yake,inanifanya nijione nimekua kwa kiasi fulani’

‘Siwezi kusema kwa sababu nimepata tuzo leo nilikua nafanya show Milion 3 basi kuanzia leo nianze kufanya show Milion 6 Milion 5,kazi zetu zinaenda na makubaliano wakati mwingine zinategemea na umbali unaweza kufanya hapa Dar ikawa tofauti na ukienda kufanya show kanda ya ziwa,hii ni biashara na biashara yangu ina makubaliano zaidi’- Dayna Nyange

Comments

comments

You may also like ...