Header

Okwi aomba jezi ya Kichuya

Winga wa klabu ya SC Villa ya nchini Uganda  Emmanuel Okwi ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri toka ajiunge na timu hiyo akitokea nchini Denmark ameweka wazi nia yake ya kutaka kurejea tena kwa Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club

Okwi amekiri kuwa akifuatilia sana viwango vya wachezaji wa Simba na amekubalia uwezo wa Shiza Ramadhani Kichuya pamaoja na anachofanya uwanjani na kwamba yeye akitua wakiunga basi moto utawaka.

“Kwanza na mpongeza Kichuya kwa kazi nzuri anayofanya uwanjanina klabu ya simba kwa ujumla na pia anaitendea haki jezi yangu kwani anafunga magoli muhimuna namuombea mafanikio kwenye soka lake lakini siku nkija Simba ntokamuomba aniachie hiyo jezi“Amesema Okwi akizungumza na gazeti la Mwanaspoti

Okwi anapenda kuvaa jezi namba 25 kwa kuwa ni siku yake kuzaliwa ila pia anavutiwa sana namba 14 sababu ya kumpenda sana Winga wa kifaransa Thiery Henry

Comments

comments

You may also like ...