Header

Ray Kigosi amtolea uvivu Wema Sepetu

Ama kweli kwenye tukio kuna mengi hutokea!! Baada ya watanzania kuumizwa tukio la kutekwa kwa wasanii wa Muziki wa Hip Hop Roma na Moni kutekwa juzi usiku leo wasanii wawili wakubwa kwenye Tasnia ya Filamu Ray Kigosi na Wema Sepetu wavaana hadharani.

Wema Sepetu alikuwa wa kwanza kuandika ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram aliowaita kuwa wasanii wa Filamu ni Wanafiki kwa hili jambo linaloendelea kwani jana walikuwa wanadai kwa mkuuu wa mkoa lakini hawakuzungumzia sakata la kutekwa kwa wasanii wenzao.

Kitu ambacho Ray Kigosi ameona ni heri amvae tuu mrembo huyo kwa kumuandikia ujumbe mreeefu uliosomeka “NAFIKIRI NI VEMA MTU KUELEZA HISIA ZAKE JAPO SIO BUSARA KWA MWENYE HISIA HIZO KUZIELEZA BILA WEREDI NAWASIHI WASANII WENZANGU KUPOTEA KWA ROMA ISIWE SABUNI YA KUTAKATISHA UCHAFU WA MTU SOTE TUMESIKITISHWA NA JAMBO HILO NA TUMEONYESHA KWA VITENDO,MIMI NIMEPOST INSHU YA ROMA TANGU JANA USIKU WEMA SEPETU WEWE ULIKUWA HUJAPOST CHOCHOTE TUSEME ULIKUWA HUNA UCHUNGU? ALAFU LEO UNAANDIKA KUWA BONGO MOVIE HAWAPO PAMOJA NA TUKIO LA ROMA HUKU NI KUTUGOMBANISHA NA WANANCHI WANAOTUAMINI. SISI BONGO MOVIE MARA NYINGI SANA TUNAKUWA PAMOJA KWENYE MATUKIO YA BONGE FLEVA TOFAUTI NA WAO. KAMA UNA UGONVI NA MTU HAYO NI MAMBO YAKO BINAFSI ILA USITUFANYE SISI TUONEKANA WABAYA MBELE YA JAMII UTAKUWA KICHAA KAMA USIPOPATA MAUMIVU KWA TUKIO LA ROMA NIMESIKITISHWA SANA POST YAKO @wemasepetu KAMA UNADHANI HUU NI MUDA MUAFAKA WA KUTAFUTIA POINT KATIKA TUKIO LA ROMA MKATOLIKI UMEFELI HILI NI JANGA LETU SOTE. @wemasepetu

Hata hivyo wema Sepetu hakuwa na chochote cha Kumjibu Ray Kigosi

Comments

comments

You may also like ...