Header

Sadio Mane kurudi uwanjani msimu ujao

Kocha mkuu wa Majogoo ya jiji  Liverpool Jurgen Klopp (JK) amethibitisha kuwa watamkosa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Msenegal Sadio Mane ambaye amaekuwa msaada mkubwa sana kwenye kikosi Liverpool.

Akizungumza na waandishi wa habari Klopp amesema maumivu aliyoyapata Mane yatemweka nje mpaka msimu huu utakapomalizika.

Mane ni mchezaji mzuri sana kama timu tunasikitika kumkosa kwa majeraha aliyoyapata yamemfanya kukosa michezo iliyosaria msimu huu lakini wachezaji wengine waliokuwa majeruhi wameanza mazoezi kama Jordan Henderson na Daniel Sturridge” Alisema Klopp

Mane aliumia kwenye mchezo dhidi ya wapinzani wao wa jadi Everton huku Liverpool wakishinda kwa magoli 3-1

Comments

comments

You may also like ...