Header

Sakata la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni latua mikononi mwa Kamanda Sirro

Baada ya kilio kikubwa kcha wasanii wa Bongo Fleva na watanzania wote kiujumla kulaani kitendo cha kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni hatimae kilio chao kimefika kwa Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda Simon Sirro.

Katibu mkuu wa Shirikisho la Wasanii Tanzania ajulikanae kwa jina la Braiton amethibitisha taarifa hizo mbele ya Waandishi wa Habari kwa kusema amewasiliana na Kamanda Sirro na amehakikisha hilo kuwa ameunda chombo maalumu kinachofuatilia sakata hilo na kesho anatoa taarifa kamili.

Mchana wa leo nimeongea na Kamanda Sirro na ametuhakikishia watu hawa watapatikana wakiwa salama na amesisitiza kuwa tuwe watulivu na tupunguze munkali wa kuilaumu Serikali”Amesema Braiton.

Alieendelea kwa kusema “Simon Sirro ametuhakikishia hilo kwamba ameunda chombo maalum na ametuahidi kesho saa tano na nusu tufike ofisini kwake kupata taarifa kama amewapata au kuna chochote kimepatikana

 

Comments

comments

You may also like ...