Header

Waarabu watua Dar es Salaam kimya kimya kuwakabili Yanga

Klabu ya MC Alger ya Algeria imewasili nchini salama usiku wa leo tayari kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho Jumamosi.
MC Alger wametua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na baadhi ya maofisa wa ubalozi wao nchini.
Yanga watakuwa wenyeji wa waarabu hao Jumamosi na imeelezwa wataweka kambi kwenye Baraza la Maaskofu eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam,Kikosi cha MC Alger kimetua jijini Dar es Salaam na wachezaji wake wakionekana kujiamini tayari kwa mechi hiyo.

Comments

comments

You may also like ...