Header

Mchezo wa Mbao FC na Simba wapigwa kalenda

Baada ya kushuhudia mabadiliko ya uongozi kwenye msimamao wa ligi kuu Tanzania Bara kupamba moto na vita ya kuepuka kushuka daraja wiki iliyopita Ligi  inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo sita mbali mbali.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo leo Mbeya City itavaana na Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Majimaji ya Songea itaialika African Lyon ya Dar es Salaam kwenye dimba la Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma mechi nyingine kwa siku ya leo  itakuwa ni kati ya Kagera Sugar na JKT Ruvu  siku ya jumapilii Stand United itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons

Baada ya hapo Ligi inatarajiwa kuendelea Jumatatu Aprili 10 kwa michezo miwili ambako Simba itakuwa mgeni wa Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mchezo huu mwanzo ulipangwa kupigwa leo huku Mtibwa Sugar itaialika Azam FC kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

 

Comments

comments

You may also like ...