Header

Mecky Maxime autamani ubingwa

Kocha mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime ameibuka na kutuma salamu kwa  kuwa JKT Ruvu wajipange vizur kwani hatakuwa na msahama hii leo kwani amejipanga kuakikisha anapata pointi tatu.

Mecky ameiambia DizzimOnline anaamini ushindi wao katika mchezo dhidi ya Simba utakuwa kichocheo cha cha timu yake kuitungua JKT Ruvu katika mchezo huo.

 “Nashukuru kuona timu yangu inazidi kupata mafanikio, haya ni matunda yanayotokana na mipango tuliyojiwekea toka awali, lengo letu kwa sasa ni kuona tunashinda michezo yetu iliyosalia ili tumalize ligi tukiwa kwenye nafasi tatu za juu,” alisema Mexime

Kocha huyo wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema anaamini mpaka sasa nafasi ya Ubingwa ipo kwa timu yoyote iliyonafasi za juu

Comments

comments

You may also like ...