Header

Rapa AKA ashindwa kutumia nyimbo zake

Rapa AKA a.k.a Super Mega anayefanya vizuri na wimbo wake mpya inayokwenda kwa jina ‘The World Is Yours’ aonekana kuwa tofauti katika kutumia nyimbo zake katika nafasi zinazomruhusu kufanya hivyo.

Akiwa nchini Kenya kwa ajili ya tamasha lake amesema kuwa mara zote hatumii muziki wake kama ringtone inagawa ukimpigia unaweza kusikia sauti ya baadhi ya nyimbo zake.

“Noo… i dont use my music as a ringtone on my phone…but when people call me they hear my own music” Alisema AKA alipokuwa akihojiwa katika kituo cha Tv cha NTV.

Hata hivyo AKA na Cassper Nyovest ni wasanii wa muziki wa rap wenye ushindani mkubwa na mwezi Octoba mwaka jana walionekana kumaliza tofauti yao jambo ambalo wengi ndani na nje ya Afrika Kusini walionesha kupendezwa nalo. Alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na rapa Cassper alisema kuwa hakuna tofauti kati yao na alipulizwa kama kunaweza tokea wawili hao kufanya kazi ya pamoja alijibu kuwa haiwezekani kabisa.

Comments

comments

You may also like ...