Header

Victor Moses arejea dimbani

Meneja wa Chelsea Muitaliano Antonio Conte amebainisha kuwa Victor Moses yuko mbioni kucheza mchezo wa leo wa Ligi Kuu Uingereza  dhidi ya Bournemouth baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbu

Moses alirejea mazoezini Alhamisi mchana na kwa sasa ni sehemu ya kikosi cha The Blues ambacho leo kitaumana na Bournemouth mchezo utapigwa uwanja wa Vitality hii inamaanisha Conte sasa na uchaguzi mpana wa wachezaji kwa ajili ya mechi hiyo

Alifanya mazoezi na sisi jana na leo lakini bado nahitaji kuangalia hali yake ili kufanya maamuzi sahihi Sasa yupo tayari Hakuna majeraha mapya kwenye kikosi chetu” aliwaambia waandishi wa habari Conte

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria amezikosa mechi mbili za Chelsea tangu kipindi cha mapumziko ya kimataifa baada ya kupata majeraha madogo ambayo awali ilihofiwa yangehitaji tiba ya upasuaji.

Comments

comments

You may also like ...