Header

Baada ya Joh Makini sasa ni Jah Prayzah na Davido

Msanii kutoka Nigeria na hitmaker wa ngoma ‘If’ iliyotayarishwa na mkali mwenzake ‘Tekno’ kila anapomkubali msanii kimuziki na kiabishara na akaweza kumkaribia kwa mazungumzo basi hasiti kuweka mazingira ya kufanya kazi. Imeshatokea kwa wakali kama Nasty C kutoka Afrika Kusini, tukaona kwa Joh Makini kutoka Tanzania na sasa imetokea kwa Jah Prayzah kutoka Zimbawe.

Kupitia video inayoendelea kusambaa hitmaker wa ngoma ‘Watora mari’ na ‘Sendekera’ aliyowashirikisha Mafikizolo, Jah Prayzah alionekana katika video ya kujishoot(selfie) akiwa na Davido video iliyothibitisha kuwa wawili hao wako katika utaratibu wa kufanya kazi ya pamoja.

“mambo yanendelea Nigeria na Zimbabwe tunakaribia kufanya kitu kibuwa wazimu” Alisema Davido akiwa na Jah Prayzah katika Video hiyo.

Hata hivyo kwasasa wawili hao wako Afrika Kusini ambako kuna uwezekano mkubwa kazi hiyo ikafanyika nchini humo ili kuepuka usumbufu wa kukutana pamoja tena ili kufanya kazi hiyo.

Comments

comments

You may also like ...