Header

Mama Moni Centrozone amtaka mwanae aachane na muziki

Ni tukio lilosikitisha wengi ya kutekwa kwa wasanii Roma, Moni Centrozone na wenzake tangu siku ya jumatano hatimaye jana zilitoka taarifa za kupatikana kwao na wakiwa salama kupelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay kilichopo jijini Dar es salaam kwa mahojiano kisha kupelekwa hospitali ya Mwananyamala kwa lengo la kuhakiki sualam wa afya zao.

Kwa mujibu wa Bi. Fatma Seleh ambaye ni mama mzazi wa msanii Moni Centrozone amesema kuwa kutokana na tukio la utekaji lililotokea na kuhusika kwa mtoto wake amehaidi kuzungumza naye atakapotoka katika suala hili na atamshauri aachane na muziki na ajihusishe na mambe mengine kwasababu kama ni elimu anayo kwakuwa hajaona mafanikio aliyoyapata kutokana na muziki zaidi ya nguo,simu na viatu.

Msikize mama mzazi wa Moni katika mahojiano na Dizzim Online.

 

Comments

comments

You may also like ...