Header

Manchester United yaiangamiza Sunderland

Matumaini ya Sunderland yamezama kwa mara nyingine mara baaada ya kuchabangwa na Manchester United mabao 3 patupu ushindi huo ulioiweka Man U katika nafasi ya tano.

Katika mchezo Sunderland ilicheza na kikosi cha wachezaji 10 kufuatia Sebastian Larsson kupewa kadi nyekundi alipomchezea vibaya Ander Herrera.

Wakati huo Zlatan Ibrahimovic alikuwa taraia ameiweka Mancheter United kileleni kwa bao moja.

Henrikh Mkhitaryan aliifunga bao la pili huku naye Marcus Rashford akifunga bao la tatu.

Sunderland wanatafuta pointi 10 kujiokoa kutimuliwa kutoka ligi huku wakiwa na mechi 7 pekee za kucheza wakiwa hawajafunga goli katika mechi saba.

United, wamewapindua Arsenal wakiwa pointi nne nyuma ya Manchester City.

Comments

comments

You may also like ...